Uanishaji ni njia ya kuweka lugha katika makundi Kwa kuongozwa na vigezo mahususi.Mgullu (1999), anasema kuwa uainishaji wa lugha unaweza kufanywa kwa kuzingatia vigezo mbalimbali ambavyo ni uainishaji wa lugha kinasaba, uainishaji wa lugha kijiografia, uainishaji wa lugha kiuamilifu na uainishaji wa lugha kimuundo/ kimofolojia.
Vigezo vya kuainisha lugha
Kinasaba
Kijiografia
Kimuundo/ kimofolojia
Kiuamilifu/Kiutendakazi
1.Uanishaji lugha Kinasaba
Ni mchakato wa kuweka lugha zinazotokana na lugha mame Moja katika Kundi moja. Lugha zinazotoka na lugha mame Moja inaonyesha uhusiano na mfano mkubwa kiisimu. Uainishaji wa lugha za kibantu ulizingatia uanishaji huu. Lugha za kibantu zilitoka Kwa lugha mame Moja ambayo ni Proto-Bantu. Mifano mengine ya kimataifa, mathalan Indo-European languages na American -Indian Languages. Wanaisimu Greenberg na Guthrie walifanya utafiti kuonyesha unasaba baina ya lugha ya Kiswahili na lugha zinginezo za kibantu. Walipata kuwa;
Walichunguza asili ya neno ‘bantu’ au ‘muntu’ Kwa uwingi. Shina hili la neno limetapakaa katika lugha nyingi za kibantu mathalan; Mtu-watu-kiswahili, Muntu-antu-Kimeru, mûndû-mûntû- Kikuyu n.k
Lugha hizi Zina muundo wa silabi wazi yaani KVKV.
Lugha hizi hufuata mfumo wa ngeli.
Mofolojia Ina muundo wa kiima na Kiarifa.
Maneno zake zinaweza kuambishwa
Maoni hii ya kiisimu inaonyesha unasaba wa lugha za kibantu.
2.Uanushaji wa lugha kijiografia .
Uainishaji wa lugha kijiografia ulikuwa unazingatia zaidi mahali au eneo ambapo lugha fulani huzungumziwa mathalani lugha za Kibantu zinavyoainishwa tunaona kuwa uainishaji huu ulikuwa ukizingatia kigezo cha mahali, mfano kulikuwa na Kibantu cha Mashariki, magharibi, kati na Pwani Nchini Kenya.
3 Uainishaji wa lugha kiuamilifu
Inahusu utendakazi wa lugha/Jukumu ya Kila lugha katika jamii, nchi na kimataifa.
Katika uainishaji wa lugha Kiuamilifu au matumizi ya lugha wataalamu wameweza kuzipa lugha majina mbalimbali kulingana na namna lugha hizo zinavyotumika au kufanya kazi; mathalan,
Lugha rasmi, ni lugha inayotumika katika shughuli zote rasmi au za kiofisi, kuandika stakabadhi, shuleni n.k
Lugha ya kitaifa , ni lugha ambayo imeteuliwa na nchi Fulani Ili kuwaunganisha watu k.v Kiswahili nchini Kenya.
Lugha mame ni lugha ambayo lugha zingine zimechipuka kutokana nayo k.v Proto-Bantu.
Lingua franka ni lugha ya mawasiliano, huibuliwa baina ya watu wanapozungumza lugha tofauti tofauti.
Lugha ya kwanza ni lugha ambayo mtu huipokea Kwa wazazi wake au katika mazingira asilia.
Lugha ya pili ni lugha ambayo mtu hujifunza-Kirasmi- baada ya kupokea lugha ya kwanza.
Lugha kadirifu ni lugha yenye matatizo mengi inayotokea wakati mtu anajifunza lugha ya pili.
Lugha lengwa, ni lugha ambayo mtu anakusudia kupata ujuzi wake/Kujifunza
Pijini ni lugha ambayo inabuniwa Ili itumike baina ya watu wenye lugha tofauti na Hawana lugha Moja ya mawasiliano.
Krioli ni pijini iliyokomaa , kupata wazawa asilia n.k
- Uanishaji wa lugha kimuundo/Kimofolojia
Inahusu kuainisha lugha Kwa kuzingatia miundo ya maneno ya lugha hizo.
Mgullu (1999) anasema kuwa uainishaji wa lugha kwa kutumia kigezo hiki cha Kimofolojia umeainisha lugha kwa kuzingatia au kutumia miundo ya lugha mbalimbali za jamii. Kutokana na uainishaji huu tunapata aina hizi za lugha;
Lugha Ambishi
Lugha Ambishi ni lugha ambazo maneno yake huweza kuongezwa viambishi. Kiswahili ni lugha Ambishi. Viambishi vinaweza kuwa awali kabla ya mzizi na tamati baada ya mzizi wa neno au kitenzi.
Lugha Tenganishi
Ni lugha ambazo haziwezi kuambishwa wala kunyambuliwa. Huwa na mofu Moja Moja.
Lugha Ambishi- Mchanganyo, Hizi ni lugha amabazo maneno yake huambishwa na maneno hayo yanapoambishwa viambishi hivyo huchanganyika na mizizi ya maneno kiasi kwamba huwa ni vigumu kuligawa neno kwa namna ambayo inaweza kuonyesha kuwa viambishi ni vipi na mizizi ni ipi kwa sababu huwa vimechanganyika na kuwa kitu kimoja.
LughanAmbishi-bainishi, Lugha hizi ni zile ambazo maneno yake huweza kuwekewa viambishi mbalimbali. Ni tofauti na lugha ambishi-mchanganyo ambayo huchanganya viambishi vya maneno na mizizi. Katika lugha Ambaishi- bainishi mizizi na viambishi huwa havichanganyiki kwani ni rahisi kabisa kuweza kuonyesha kuwa viambishi ni vipi na mizizi ya maneno ni vipi. Viambishi hivi vinaweza kuwa vya awali au vya mwishoni/ tamati. - MAREJELEO
Mathews, P.H. ( 1991), Mofolojia ( toleo la pili) : United Kingdom. Cambridge University Press.
Massamba, D.P.B, (2009), Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam. TUKI
Massamba, D.P.B, (2002), Historia Ya Kiswahili.Nairobi.Jommo Kenyatta Foundation.
Mgullu, R.S. (1999), Mtalaa wa Isimu,Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Longhorn Publishers. Nairobi. - Obuchi, S.M. na Mukhwana ,A.(2015), Muundo wa Kiswahili, Ngazi na Vipengele. Jomo Kenyatta Foundation: Nairobi, Kenya
TUKI (1990), Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha. Dar es S alaam: TUKI

Leave a comment