Lugha ni mfumo wa sauti na ishara za nasibu inayotumika jamii yenye utamaduni wao kwa mawasiliano.
Mfumo ina inadhihirisha kuwa lugha ina safu mbili kuu:
Maana
Sauti
Kila lugha ina fonolojia/sauti zake za pekee. Sauti mbalimbali hubainishwa na sifa mbalimbali.
Lugha ya binadamu pia hutumia ishara, kuna ishara za aina mbili:
Ishara za nasibu, ambazo hakuna uhusiano baina ya kitaja na kitajwa, mathalan; meza, kiti n.k
Ishara zisizo za nasibu, hapa kuna uhusiano baina ya kitaja na kitajwa, mathalan; tuktuk, Tingatinga n.k
Lugha hukitofautisha binadamu na Wanyama; sifa bia za lugha- inahusu sifa za lugha za binadamu ambayo hukitofautisha na Wanyama. Sifa hizo ni kama vile;
Umakinikaji, lugha humwezesha binadamu kuweza kuzungumza/ kujihusisha na mawasiliano hata ijapokuwa anajishughulisha na kazi zingine. Tofauti na Wanyama ni lazima wajishughulishe kikamilifu na shughuli zao, mathalan nyuki, ngombe n.k
Unasibu, inadhihirisha uhusiano baina ya kitaja na kitajwa, kiashiria na kiashiriwa. Kuna maneno mengi sana katika lugha ambayo hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kitaja na kitajwa kwa mfano, nyumba, mbwa, shule n,k hata hivyo kuna yale ambayo hudhihirisha uhusiano huo k.v tuktuk, pikipiki n.k
Kuongopa, lugha humwezesha binadamu kusema uongo, hata hivyo kuna kiwango kidogo ambapo Wanyama huonyesha uwezo huu kwa mfano; jogoo
Uzalishaji/ ubunaji, lugha ya binadamu humwezesha kuzalisha kauli nyingi zisizo kikomo kwa kuzingatia kanuni ya lugha husika.
Uhamishaji, lugha humwezesha binadamu kutoa kauli za wakati uliopita na pia kauli ambazo zitatimizwa baadaye.
Utamaduni, lugha hutumika na wanadamu wenye utamaduni mahususi, kila jamii hutumia lugha kulingana na kanuni walizoweka. Wanyama hawana utamduni.
0717558214- NICHOLAS ROP KIPLANG’AT

Leave a comment