Hili si jambo la milele nililotamani,
Mawimbi haya makali, naona Maisha tuliumbiwa kuteseka na kuteswa tu…
Natafuta faraja popote nionapo panapo,
Chini ya mbuyu natulia, utulivu wa fikra tu,
‘Hii Maisha ungebadilisha iwapo ungeelewa maneno hayo, ukweli usiojua ni kuwa-Sitoweza kusahau, wino wa maneno yako isofutika’
Mwishowe, nahisi uzito tu ndani ya moyo wangu,
Naona dunia sikuumbiwa mimi!

Kumbukumbu nzuri zaidi zinaweza pia kuharibiwa, kwa sababu ya neno moja tu.
Usiseme chochote kwa kuwa umezoea mimi niseme, najaribu kuelewa iwapo waelewa mambo haya lakini hueleweki hata nikilewa,
Kwa mara nyingine tena, Usiku wa kimya!

Umevunjavunja moyo wangu,
Inakuwa vigumu kubeba inapovunjwa vipande vipande milioni moja,
Kwa hivyo labda ifunge tu yote pamoja na kuondoka…
Una bili za kulipa na maisha ya kuishi,
Huenda usipate muda wa kutosha wa kulia au kuhuzunika ipasavyo,
Lakini utawezaje kuhuzunika? Ulikuwa na muda wote wa kubadilisha haya!

Inachukua nguvu nyingi kushikilia kile ambacho hakikusudiwa kuwa,
Hasira zangu zamwendea aliyepanga tukutane hapa, tujuane, kuweka hisia zangu kwako na yeye mwenyewe alijua mambo haya hayatawezekana,
Angalia unavyofariji wengine kwa maneno unayotaka kusikia…
Samahani mambo yamekuwa hivi,
Naona ni bora kulazimisha, barabara hii iliyo Tofauti.
Najua hukuwa tayari; lakini hapakuwa na mahali pa kujificha.
Najua ulitaka kupiga mayowe, lakini ulichoweza ni kuhema sana.
Nimeandika yote juu yake, katika barua ambayo sikuwahi kuchapisha, nakala yake inapatikana moyoni mwangu na kopi yake unayo ubongoni mwako.
Hakuna mtu aliyekuwepo wa kusema siri.

Hii sio milele niliyoota.
Hii sivyo nilivyodokeza
Maisha ya taabu isiyo na mwisho.
Maisha ya kwaheri zisizotarajiwa.


Leave a comment