Sikio la Mama!

Katika kijiji kimoja cha Sikujua, kulikuwa na familia moja, baba, mama na mtoto wao mmoja aliyeitwa TikTok. TikTok alikuwa kijana mwenye busara na heshima, lakini ghafla tatizo la kifamilia likatokea. Waliosema na walisema: “Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, na kuzaa mwana si kazi, bali kulea ndio kazi.” TikTok alipofanya kosa na baba yake akataka kumwadhibu mama yake, alijitokeza na kusema, “Mwache, nitamlea mimi.” Tena, alipofanya kosa na mama yake alitaka kumwadhibu baba yake, naye akadakia kusema, “Mwache, nitamlea mtoto wangu.”

Kutokana na hali hiyo ya kimalezi, TikTok akageuka kuwa mtoto mjeuri na mwizi sugu. Akaanza polepole kuiba vitu vya nyumbani, kisha akawa mwizi hatari asiyekuwa na huruma.

Inasemekana siku za mwizi ni arobaini, hivyo TikTok alikamatwa na polisi. Akapelekwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka. Kesi ilipoamuliwa, ikabainika kuwa TikTok atafungwa gerezani maisha yake yote! TikTok alikubali matokeo hayo, ila akaomba kuzungumza na mamake.

Alipomwita mamake, alimgeukia kwa upole, lakini ghafla alimng’ata sikio. Kisha akazungumza kwa ukali huku damu ikimdondoka kinywani akisema, “Ewe mama, ulikuwa na wakati mzuri wa kunilea, ila kila wakati mligombana juu ya nani atanilea, lakini hamkunilea kamwe!”



Leave a comment

About Me

Welcome to my blog, MTU KUZI, a space dedicated to informing and educating a diverse audience without bias toward age, gender, race, or any other distinguishing factor. I am a seasoned professional with a deep foundation in communication, translation, administration, and education. My extensive experience spans prestigious roles at institutions like Pwani University, Mozilla Foundation, KIPPRA, and teaching Kiswahili at the University of Carolina – Chapel Hill.As a Kiswahili expert, I specialize in translating between English and Kiswahili and tutor both languages with a focus on immersive, practical learning experiences. My expertise in Kiswahili not only enhances my teaching but also enriches my translations, allowing for culturally and contextually accurate communication.In this blog, I leverage my skills and experiences to create content that bridges cultural divides and fosters understanding. Proficient in various software applications and online collaboration platforms, I aim to streamline communication processes and engage with a global audience effectively.You are invited to join me on this journey of exploration and learning. Follow MTU KUZI on Facebook, Twitter, Instagram, and LinkedIn to stay updated and connected. Thank you for visiting, and I look forward to sharing more with you.

Newsletter