ASILI YA JAMII YA KALENJIN!

Utamaduni inahusu Mila, asili, mitazamo na desturi au Maisha ya jamii Kwa jumla. Kama tunavyojua utamaduni ni nyenzo muhimu sana katika kulea lugha Fulani, jamii nayo huipa lugha jina na eneo la linalotumika. Utamaduni huonyesha shughuli za Kila siku za jamii Fulani. Kalenjin ni Jamii kubwa inayounganisha lahaja mbalimbali, mojawapo ya lahaja hiyo ni Kipsigis. Kipsigis wanapatikana katika maeneo kama vile Bomet, Kericho na Nakuru hata hivyo kutokana na maendeleo ya jamii na uchumi wanapatikana sehemu mbalimbali nchini Kenya na hata nchi za nje. Ili kuelewa utamaduni wa Kipsigis nitaeleza kadri ya Uwezo wangu asili yao, Mila,desturi na mambo mengine yanayohusiana na utamaduni wa Kipsigis.

Hapa nitaelezea harakati za watu wa Kaleniin hadi walipo sasa. Kaleniin ni miongoni mwa jamii ya Kiniloti za Nyanda za Juu nchini Kenya. Wanachukua sehemu kubwa za bonde la ufa. Baada ya Mungu kuumba wanadamu wa kwanza kizazi kilikua mpaka wakati wa Yesu hadi alipopaa mbinguni. Tangu wakati huo wanadamu walikua na kuendelea Kwa Kasi.
Watu wote waliondoka Misri na kundi mojawapo lilikuwa ni Kaleniin. Walipotoka Misri, waliongozwa na mtu/mzee aliyeitwa Miot. Mto Nile ikawa kama dira yao, walifuata kingo zake kuelekea Afrika. Walifika mahali ambapo ziwa Viktoria inaungana na kuunda mto Nile. Miot alikuwa na wana watano na binti mmoja. Walipata njia ya kuelekea Mlima Elgon kupitia ziwa Albert na Kyoga. Wakiwa njiani waliwaacha baadhi ya watu wao ambao sasa wanazungumza lugha nyingine(huko Sudan).
Walikaa katika eneo la Mlima Elgon kwa muda fulani lakini jambo la kwanza walilofanya ni kuwatahiri wavulana wa kwanza kwa sababu walikuwa wamezeeka kwani walikuwa wamesafiri kwa muda mrefu. Zoezi hilo lilifanywa na Miot mwenyewe. Miongoni mwa waanzilishi ni mwanawe mkubwa wa Miot aliyeitwa Sabaot, ambaye baadaye aliachwa katika Mlima Elgon kuendeleza ukoo huo wa Sabaot.
Wakati huo ndipo Maasai fulani aitwaye Solacha/Sulacha alikuja. Alimwomba Miot amruhusu kuoa binti yake (mtoto wa kwanza wa Miot na binti wa pekee). Kwa kuthamini na kama shukrani hili Solacha alimpa Miot ng’ombe na ndama pamoja na Sotet( chombo muhimu sana Katika utamaduni Wa Kipsigis). Alimwagiza Miot kwamba kibuyu hicho alipaswa kutumia yeye na mkewe wakati wa kunywa maziwa wakati watoto wanapaswa kutumia majani ya miti.
Miongoni mwa wana wa Miot walikuwa Sabaot, Nondin(Nandi), Kipsigisin, Keiyo na Tugen. Miot, wanawe na watu wengine walikaa Mlima Elgon kwa muda mrefu kabla ya kusafiri Katika harakati ya kutafuta malisho mapya. Waliondoka Sabaot na watu wachache na mifugo wao. Sabaot akaunda kabila la kwanza.
Miot akiwa na watoto wake na watu wengine walianza safari ya kuelekea eneo la kwanza lililoitwa Katani lel (Kitale) kwani kulikuwa na miti nyeupe ya Acacia. Baadaye walihamia Lel Teret(Eldoret) iliitwa hivyo kwani walitengeneza jerrycan/Vyungu vyeupe. Pia walihamia Tim-borowa (Timboroa) iliyopewa jina hilo kutokana na kuwepo Kwa miti fulani inayopanda nyingine, miti hii inaweza kutumika wakati wa kujenga. Kutoka hatua hii walisafiri hadi Tulwap Kipsigis(Mlima wa Kipsigis/Kilima).
Wakiwa Tulwap Kipsigis kundi la wavulana wakubwa walitahiriwa na kutengwa ili kupata nafuu. Kwa mbali waliona moshi, wakafikiri walikuwa ni Wamasai, wakaenda kuvamia mifugo yao. Wamasai walikuja kulipiza kisasi baadaye, waliposikia hivyo Miot na watu wake walikimbia wakiwaacha wale watahiriwa nyuma. Kwa bahati mbaya wote waliuawa na Wamasai. Kwa hiyo milima hiyo iliitwa Tulwap lagoi (Kilima/mlima wa watoto/wavulana) au Tulwap Ngetik( Kilima/mlima wa wavulana wasiotahiriwa). Miot na watu wake walikaa huko kwa karibu miaka 90 wakitaja koo zote za kalenjin. Ukoo wa kwanza ulikuwa Maina, Chumo,Sawe,Korongoro, kaplelach,kipnyige na Nyongi. Katika hatua hii mtoto wa pili Nondin(Nandi) aliamua kutafuta malisho mapya. Alikwenda Tinderet na watu wachache na mifugo kama ilivyokuwa desturi. Kipsigis alikwenda Chepsir. Huko Chepsir walipanda mtama baada ya moto kuteketeza kila kitu, kulikuwa na mavuno mengi ambayo hakukuwa na vifaa vya kuhifadhi, walitengeneza Kisiet na kwa hivyo jina la Kipsigis likaja kuwa hai(Kipsigisiet/Kipsigis). Keiyo alihamia sehemu za Timboroa. Tugen alikuwa mtoto wa mwisho na mdogo wa Miot kuhama.
Inasemekana wakiwa njiani Tugen alinaswa na Keiyo na kuvunja kibuyu alichokuwa amepewa Miot na Sulacha. Kwa hivyo Miot aliwaachia laana kwamba Tugen ataishi milele katika maeneo yenye joto na ukame na Keiyo kwenye mabonde.
Kama mnavyojua watu wa lugha moja wanaweza kutengana na kwa hivyo lugha yao hubadilika. Hii ilitokea kwa Kaleniin pia lakini ni busara kusema kwamba utamaduni wao unabaki sawa na wao ni watu wamoja. Swali lingine la kujibu ni kwamba watu wa Marakwet na pokot walikuja kuzaliwa kutoka kwa Keiyo. Ogiek walizaliwa kutoka Kwa Kipsigis. Tulwap Kipsigis (Kilima/mlima wa Kipsigis) ni sehemu mbili za juu kabisa ambazo zilikuwa za wanaume na wazee na ndogo zaidi ilikuwa ya wanawake na Watoto.



Leave a comment

About Me

Welcome to my blog, MTU KUZI, a space dedicated to informing and educating a diverse audience without bias toward age, gender, race, or any other distinguishing factor. I am a seasoned professional with a deep foundation in communication, translation, administration, and education. My extensive experience spans prestigious roles at institutions like Pwani University, Mozilla Foundation, KIPPRA, and teaching Kiswahili at the University of Carolina – Chapel Hill.As a Kiswahili expert, I specialize in translating between English and Kiswahili and tutor both languages with a focus on immersive, practical learning experiences. My expertise in Kiswahili not only enhances my teaching but also enriches my translations, allowing for culturally and contextually accurate communication.In this blog, I leverage my skills and experiences to create content that bridges cultural divides and fosters understanding. Proficient in various software applications and online collaboration platforms, I aim to streamline communication processes and engage with a global audience effectively.You are invited to join me on this journey of exploration and learning. Follow MTU KUZI on Facebook, Twitter, Instagram, and LinkedIn to stay updated and connected. Thank you for visiting, and I look forward to sharing more with you.

Newsletter