

Mwanamke Shujaa, Nelly Cheboi.
Taswira kamili inanijia akilini mwangu. Si ndoto Wala soga ya aina yoyote. Inaweza kuwa ni sadfa ila sivyo. Ni kweli wala si uvumi. Ni taswira ya mtoto wa kike, hivi Sasa mwanamke. Wanasema waswahili kuwa hata mbuyu ulianza kama mchicha. Ni katika Kijiji kisichojulikana katika eneo lolote la Afrika ama hata Kenya yenyewe. Anachipuka Nelly Cheboi.
Nelly Cheboi ni mjasiriamali wa Kenya na mfadhili ambaye amejitolea maisha yake kuboresha elimu na upatikanaji wa teknolojia kwa watoto katika nchi yake. Alizaliwa mwaka wa Elfu Moja tisini na nne na kukulia huko Kijijini Mogotio, Kaunti ya Baringo, katika familia maskini, lakini kwa bidii na kujitolea kwake, amekuwa msukumo kwa wengi. Inasemekana kuwa afadhali nusu Shari kuliko Shari kamili. Ilisadifu kuwa katika Hali hii ya kimasikini yaliyompata, yeye anapata malezi yote kutoka kwa mzazi mmoja ambaye ni mama yake. Mama yake ni Wa kisomo Cha chini na alijitolea mhanga, akijipa moyo kuwa Kuna siku ya siku ambayo Mungu atamjalia kama waja wengine. Mazingira haya ya kimasikini ndiyo ilimpa msukumo Wa kutia bidii, yeye anasema kuwa alipata msukumo mkubwa wakati alipoona mama yake akijikaza Kila wakati kwa hali na mali kuwapa chakula na masomo. Mama yake ni muuzaji Wa mboga tu Kijijini. Hii ni biashara ndogo sana ukilinganisha na mahitaji ya Kila siku ya familia. Waliishi Katika kijumba kisichokuwa na starehe yoyote. Ni nyumba ambayo wakati inaponyesha inalowa maji Kila mahali na walilazimika kusimama wakati wote. Cheboi anaeleza kuwa hawakukaribisha mgeni yeyote Katika kibanda hicho waliojisetiri ndani. Kumbukumbu za kijumba hicho kimebakia akilini mwake tu kwani hawakupiga picha yoyote nalo kutokana na Hali mbovu. Hali hii ngumu ya kimaisha inamtia Cheboi wasiwasi iwapo watoto wengine Katika sehemu zingine za dunia walipaswa kupitia Katika Hali ngumu na tatanishi ya kimaisha aliyopitia. Anaeleza iwapo Kila mtoto anapaswa kuchagua Katika ya chakula na karo ya shule, kutembea bila viatu, kustahimili dharau ya jamii na mambo mengine mengi yanayokatiza maini.
Nelly Cheboi hata hivyo anapata tumaini na mshawasha mkubwa Wa kuendelea kutokana na bidii aliyokopa kutoka kwa mama yake. Anaamini kuwa kutokana na bidii yake Katika masomo anaweza kubadilisha maisha yao. Anakumbuka wimbo aliyomwimbia mama yake Kila wakati na iliyomtia moyo sana,
‘ Mikono yangu midogo wee, haiwezi kufanya kazi
Nikiwa mkubwa wee, nitakusaidia
Utapumzika.’
Nelly ni mtoto wa mwisho kati ya watoto sita katika familia maskini, na mzazi wake alitatizika kuhudumia watoto wake. Licha ya hali yao ngumu, mzazi wa Cheboi aliwapa watoto wake motisha ya kupenda elimu na imani katika uwezo wa kufanya kazi kwa bidii.
Cheboi alikuwa mwanafunzi bora na mwenye bidii sana,alifaulu shuleni na aliazimia kuendelea na masomo zaidi ya shule ya upili. Hata hivyo alipitia changamoto nyingi za kiusomi hapa na pale. Anaeleza kuwa kutokana na ukosefu Wa taa alienda Katika hospitali iliyo katibu na kusoma mpaka saa nane za usiku huku akifyonzwa damu na mbu. Mungu hamwachi mja wake na pia mchumia juani hulia kivulini, Cheboi alifaulu na akawa msichana na mwanafunzi bora Katika eneo la Koibatek. Alijiunga na shule ya … Nairobi. Hata hivyo, matatizo hayakuisha Bali yalianza upya Katika mkondo mwingine, aliishi kwa chakula Cha shule pekee na hakuwai kununua hata mandazi Katika duka shuleni kutokana na ukosefu Wa hela. Pia aliweza kutumwa nyumbani mara Kwa mara kutokana na karo. Wakati huo nauli ilikuwa takriban shillingi mia tank ambayo hangeweza kumudu na alitatizika sana. Aliporudi nyumbani alibeba vitabu vyake vyote ili asome wakati alipokuwa akimsaidia mama yake Katika kibanda yake ya mboga na kupika vyapati. Hata hivyo, alijitahidi na aliweza kukamilisha shule ya upili akiwa na alama ya ‘A’ Katika Kila somo. Alirudi nyumbani na kutokana na Ari yake ya kuendelea na masomo alipenda kujieleza Kwa watu kuwa alisimomea shule Fulani na alipata alama ya juu zaidi, hii ilimfaidi zaidi na akapata habari kuhusu zawadi Afrika inayowapa wasichana ufadhili Wa masomo. Baada ya Kupata ufadhili huu, Cheboi hakuwai na vifaa na stakabadhi zinazohitajika kusafiri kwendaa marekani. Hivyo akarudi Tena mtaani na wimbo wake aliouzoea, ‘ Mimi ni Cheboi, nilisomea shule ya… ,nikapata alama ya juu, nimepata ufadhili ila nimekosa visa na passport’. Baadaye alifanikiwa Kupata haya yote na alikuwa tayari kusafiri akiwa na jambo Moja akilini kubadilisha maisha yake , familia yao na watu wengine. Kwa msaada wa ufadhili wa masomo kutoka Zawadi Afrika, aliweza kusoma sayansi ya kompyuta katika Chuo cha Augustana huko Illinois, Marekani. Mwacha Mila ni mtumwa, Nelly hakusahau yaliyomngoja nyumbani kwao. Alijizatiti Kwa kufanya kazi ya kuosha choo shuleni mwake, hata wakati Wa likizo alibaki pekee akifanya kazi Kwa muda wote. Alikusanya fedha alizopata akanunua sehemu ya shamba Kwa minajili ya kujenga shule. Pia alirudi akajengea familia yake jumba nzuri yenye vyumba vitatu na Samani. Familia yake ikafurahi na mamake akakumbuka Ile wimbo ya Nelly kuwa wakati huo mikono yake midogo haingeweza kumsaidia ila Sasa ana uwezo huo. Alihitimu mnamo mwaka Wa Elfu mbili na kumi na tano akiwa na Shahada ya Sayansi ya Kompyuta.
Baada ya kuhitimu, Cheboi alianza kazi yake kama mchambuzi wa biashara na mhandisi mkuu wa programu kwa makampuni mawili ya Marekani – New World Van Lines na User-Hero. Haraka alipata sifa ya kuwa mfanyakazi hodari na aliyejitolea na aliheshimiwa sana na wafanyakazi wenzake.
Licha ya mafanikio yake nchini Marekani, Cheboi alidhamiria kutumia ujuzi wake kuleta mabadiliko katika nchi yake. Mnamo mwaka Wa Elfu mbili na kumi na tisa, alichukua uamuzi wa kuacha kazi yake ya kulipwa na kurudi Kenya kuanzisha kampuni yake mwenyewe.
Cheboi alianzisha ‘Technologically Literate Africa’ (TechLit Africa), kampuni inayokusanya na kurekebisha tarakilishi ili kuunda maabara za teknolojia na tarakilishi shuleni. Kampuni hiyo inalenga kuwapa watoto katika maeneo ya mashambani na vijijini nchini Kenya fursa ya kupata teknolojia na intaneti, ambayo inaweza kuwasaidia kukuza ujuzi mpya na kuboresha elimu yao.
Cheboi anahudumu kama Mkurugenzi Mtendaji wa ‘Technologically Literate Africa’ (TechLit Africa) na amekuwa muhimu katika mafanikio ya kampuni hiyo. Chini ya uongozi wake, ameanzisha maabara za teknolojia katika shule kadhaa na imetoa mafunzo na usaidizi kwa walimu na wanafunzi. Ameendelea zaidi na ameweza kufungua kituo Cha kurekodi nyimbo Kwa vijana chipukizi na pia kuwafunza wasichana na wamama maarifa ya ususi bila kuulizwa cheti yoyote.
Mnamo mwaka Wa Elfu mbili na ishirini na mbili, Cheboi alitajwa kuwa shujaa wa ‘Cable News Network’ (C.N.N). wa Mwaka, tuzo ambayo inawatambua watu ambao wameleta athari kubwa kwa jamii. Alichaguliwa kutoka miongoni mwa mashujaa kumi ya ‘Cable News Network’ (C.N.N).
Cheboi alitunukiwa zawadi ya pesa taslimu ili kupanua kazi yake na TechLit Africa, pamoja na ruzuku za ziada na mafunzo ya shirika.
Katika hotuba yake ya kukubali tuzo ya shujaa wa mwaka wa ‘Cable News Network’ (C.N.N), alizungumza juu ya ushawishi wa mama yake katika maisha na kazi yake. Alisema kwamba mama yake alifanya kazi kwa bidii ili kuandalia familia yake na amewatia watoto wake kupenda elimu na kuamini kwamba kufanya kazi kwa bidii kunawezekana.
Nelly Cheboi ni mfano bora wa bidii, ushujaa na uwajibikaji kwa wanawake wote nchini Kenya na kote ulimwenguni. Mafanikio yake yanajulikana kwa wino usiofutika kwa sababu amejitolea kuwatumikia wengine kwa bidii na maarifa yake.
Kupitia kazi yake na shirika la ‘Technologically Literate Africa’ (TechLit Africa), Nelly Cheboi ameleta matumaini na mabadiliko katika maisha ya watoto wa kike na kiume katika maeneo ya mashambani nchini Kenya. Kwa kutoa fursa za kupata teknolojia na intaneti kwa watoto hawa, amewapa nafasi ya kukuza ujuzi wao na kuboresha elimu yao.
Uwepo wa Nelly Cheboi unatoa motisha na kuwapa moyo vijana wengi hususan wanawake na wasichana nchini Kenya na duniani kote. Wanapata kujifunza kuwa wanawake wanaweza kuwa wabunifu na wachangiaji muhimu katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Ni jambo la kutia moyo kwamba Nelly Cheboi ameamua kutumia ujuzi na maarifa yake kuleta matokeo chanya kwa jamii. Anaonyesha jinsi gani kila mtu anaweza kutumia ujuzi wake kuleta mabadiliko katika jamii yake na kuboresha maisha ya wengine. Ni mfano wa kuigwa kwa yeyote anayetaka kuwa na athari chanya katika jamii.
Mfano wa Nelly Cheboi unatukumbusha kuwa hakuna chochote kisichowezekana ikiwa tutaamua kufanya kazi kwa bidii na kwa moyo wote. Ni mfano wa kiongozi anayepigania usawa na fursa kwa wote, na kujitolea kwa dhati kuwawezesha watu kufikia malengo yao.
Kwa kumalizia, Nelly Cheboi ni kielelezo kwa wanawake wote kuwa wana uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Yeye ni shujaa ambaye ameamua kutumia ujuzi na maarifa yake kusaidia wengine na kuwawezesha watoto wa Kenya kufikia ndoto zao. Tuna furaha kumpongeza kwa mafanikio yake na tunamuomba Mungu ambariki katika kazi yake na maisha yake yote.

Leave a comment