TOFAUTI KATI YA LUGHA YA MAZUNGUMZO NA LUGHA YA MAANDISHI.

Uwasilishaji
Lugha ya kimazungumzo huwasilishwa kwa njia ya mazungumzo au masimulizi, lakini lugha ya kimaandishi huwailishwa kwa maandishi

Mabadiliko
Lugha ya mazungumzo hubadilika kutokana na mazingira, wahusika, mada, wakati na madhumuni yake. Lugha ya kimaandishi haibadiliki pindi tu ikishaandikwa hata kama ilikuwa na makosa mpaka ifanyiwe marekebisho upya.

Uhusiano na hadhira
Lugha ya mazungumzo huwakutanisha ana kwa ana adhira na fanani, lakini lugha ya kimaandishi haiwakutanishi ana kwa ana mwandishi na msomaji.

Maandalizi
Lugha ya mazungumzo haihitaji maandalizi makubwa ya mada, lakini lugha ya maandishi ili kutafakari mambo yatakayoandikwa na huandaa vifaa kama vile peni, penseli, rula, karatasi n.k

Uhifadhi
Lugha ya kimazungumzo huhifadhiwa kichwani ambapo huwa haidumu Kwa muda mrefu kwani alihifadhi anaweza kufa au kupata maradhi yatakayopelekea kumbukumbu kupotea, lakini lugha ya kimaandishi huhifadhiwa kwenye vitabu na sehemu nyingine ambazo huifanya kazi hiyo kudumu kwa muda mrefu.

Gharama
Lugha ya kimazungumzo haihitaji gharama nje ya ala za sauti ili kuwezesha kutamka maneno vizuri.
Lugha ya kimaandishi ina gharama kubwa kwa sababu huhitaji vifaa vya kuandikia kama karatasi, kalamu na vifaa vingine ili iandikwe kwa ukamilifu na muda.

Wahusika
Lugha ya mazungumzo ina wahusika wengi Kwa sababu haichagui wala haibagui watu fulani ndio wamiliki wa kazi hiyo kutokana na kutumiwa na watu wote wanaojua kusoma na wasiojua kusoma.

Lugha ya kimaandishi wahusika ni wachache kwani ni wale tu wawezao kusoma na kuandika.

Uhai
Lugha ya kimazunguzo ina uhai kwani huonyesha ujumbe pamoja nakuelezea hali ya mzungumzaji kama ana hasira, chuki, furaha lakini pia inawashirikisha hadhira katika vitendo mbalimbali kama kuimba, kujibu maswali n.k
Lugha ya kimaandishi ni vigumu kuonesha na kuelewa wazi hali ya mwandishikwasababu haimkutanishi hadhira na fanani ana Kwa ana.”
https://hpputumiajiwamaneno.blogspot.com/p/ofauti-baina-ya-lugha-ya-kimazungumzo.html#:~:text=TOFAUTI%20KATI%20



Leave a comment

About Me

Welcome to my blog, MTU KUZI, a space dedicated to informing and educating a diverse audience without bias toward age, gender, race, or any other distinguishing factor. I am a seasoned professional with a deep foundation in communication, translation, administration, and education. My extensive experience spans prestigious roles at institutions like Pwani University, Mozilla Foundation, KIPPRA, and teaching Kiswahili at the University of Carolina – Chapel Hill.As a Kiswahili expert, I specialize in translating between English and Kiswahili and tutor both languages with a focus on immersive, practical learning experiences. My expertise in Kiswahili not only enhances my teaching but also enriches my translations, allowing for culturally and contextually accurate communication.In this blog, I leverage my skills and experiences to create content that bridges cultural divides and fosters understanding. Proficient in various software applications and online collaboration platforms, I aim to streamline communication processes and engage with a global audience effectively.You are invited to join me on this journey of exploration and learning. Follow MTU KUZI on Facebook, Twitter, Instagram, and LinkedIn to stay updated and connected. Thank you for visiting, and I look forward to sharing more with you.

Newsletter