
Watu wengi ukiwauliza dhana ya neno Maisha hawawezi kueleza Kwa uwazi bila kutoa mifano mengi sana. Ni kweli si jambo rahisi. Wapo wataalamu wengi ambao wameona kuwa Maisha hayana maana Kwa wazo kuwa binadamu anaishi Maisha ya matatizo mengi na maisha aliyopangiwa, hivyo yeye Hana chaguo Kwa lolote linalomfanyikia. Wapo wataalamu wengi ambao wanajipa moyo kupitia Kwa dini. Kuna mambo mengi ambayo yanatufanyikia Maishani ambayo hutuacha tukijiuliza Kwa nini tupitie mambo haya magumu. Hata hivyo ni vizuri kujipa moyo na kutia bidii Kwa kazi na Imani Yako. Nitaeleza hadithi fupi ya maisha ya nzi na Buibui kuhusu dhana ya maisha.
Buibui ni mdudu Mojawapo wa wadudu katika Oda Ya Araknida, kundi la Athropodi .
Buibui hutofautiana kwa ukubwa na sumu wanaobeba hata hivyo kunao Buibui wasio hatari.Idadi kubwa ya buibui hawana madhara na hutumikia kusudi muhimu: kudhibiti idadi ya wadudu ambao wangeweza kuharibu mazao . Bila buibui kula wadudu hatari kwa kilimo, inadhaniwa kuwa ugavi wetu wa chakula ungekuwa hatarini.
Spishi nyingi ya Buibui ni walaji nyama, ama hunasa nzi na wadudu wengine kwenye utando wao, au kuwawinda. Hawawezi kumeza chakula chao mzima mzima, ingawa huwala wadudu kama nzi Kwa kuwaingiza sumu inayosaga vijisemu vya miili yao, kisha kunyonya mabaki yaliyoyeyuka.
Ingawa si buibui wote hutengeneza utando, kila spishi hutoa hariri au nyuzi Fulani ambazo tofauti na kuwasaidia kuwinda pia usalama wao, kupanda na kushuka, huwafaa kama mifuko ya mayai.

Nzi ni mdudu anayepatika mara nyingi nyumbani na popote palipo na uchafu. Nzi huleta madhara Kwa Afya ya binadamu na mifugo.

Buibui ni adui wa nzi naye Nzi ni chakula Cha Buibui. Inashangaza. Itakuwaje kifo Cha mdudu mwingine ni furaha na chakula Cha mwingine? Nzi anapopatikana pabaya na kunaswa katika nyuzi au utando wa Buibui kwanza hutatizika moyoni Kwa kunaswa hata hivyo Nzi hujipa moyo akisema moyoni ‘ … Nimenaswa ila Bado Nina uhai…’ Kwa hivyo anaendelea kupapatika huku akitaka kujinasua. Upande mwingine Buibui anacheka na kufurahi Kwa kuwa ana hakika Nzi hawezi kujinasua . Nzi anaendelea kupapatika hadi kuchoka . Buibui anajongea na kumdungia sumu ambayo husaga sehemu za ndani ya mwili wa nzi. Baadaye hunyonya. Anajishibia na kuenda zake kungoja windo wa siku nyingine. Kinachobaki Kwa nzi ni ule ngozi au sehemu ya juu inayositiri sehemu za ndani ya mwili wa nzi.
Lakini, ni Kwa nini Buibui anafurahi na amemuua mwenzake? Na Je, Nzi asiponaswa si Buibui atajifia Kwa njaa? Sasa Maisha ni nini?


Leave a comment