
Mara nyingine unachokiamini na kinachoendelea kwenye maisha yako huwa ni vitu viwili tofauti kabisa.
Unamaamini katika kuwa mtu mkuu lakini kwa leo hakuna anayekuamini,unaamini kuwa mfanyabiashara mkubwa lakini hauna mtaji wa kuanzia,unaamini katika kuwa mtu mwenye ushawishi lakini leo hakuna mtu aliye tayari Kuamini na kukupa fursa hata ndogo tu.
Moja ya nyakati ambayo wengi huipoteza ndoto yao ni pale ambapo wanachokiona ndani yao hakifanani na kinachoendelea nje yao. Usisahau hiyo ni kanuni ya kawaida ya Maisha, Kuanza kuishi ndoto yako ndani kabla haujaishi nje yako kwanza.
Kitu kikubwa ni kuendelea kuamini kuwa unawez na kuchukua kila hatua inayowezekana kwa wakati huo.
Usiache kuwa na mipango mikubwa eti kwa sababu mazingira yanaonekana yamegoma, La hasha! Endelea na mipango yako kama kawaida. Thomas Edson Aliwahi kusema “When a man puts limit on what he Will Do, He has put a limit on What He Can Do” .
Kuwa na Mipango mikubwa na kuamini katika kufanya makubwa katikati ya Changamoto hakutakugharimu chochote.

Leave a comment