Machi 28, 1980; Kikundi cha wanaelimu chimbo(archaeologists) ikiongozwa na Simon Gypson na Professa Amos Kloner waligundua makaburi ya zamani sana. Makaburi haya yalikuwa na majeneza na ndani yake mifupa ya watu waliozikwa humo. Majeneza hayo yalitengenezwa kwa udongo ngumu na Wayahudi. Wayahudi waliita Ossuary.
Mabaki hayo yaligunduliwa katika mji mdogo wa Talpiot(Talpiot Tomb) umbali wa maili tatu hivi kutoka Yerusalemu.




Makaburi hayo yalikuwa ya karne ya Kwanza katika enzi za Yesu. Huo ulikuwa mtindo wa kuzika watu miaka thelathini kabla ya Yesu na ukaendelea kwa miaka sabini baadaye wakati wa uwepo wa Kristo.
Kugunduliwa kwa makaburi hayo ulisimamisha shughuli ya ujenzi uliokuwa ukiendelea na yale majeneza ya udongo mgumu yalipelekwa katika makumbusho makubwa ya kihistoria mjini Yerusalemu kulikoitwa Rockerfeller Museum ili kufanyiwa utafiti wa kisayansi na kihistoria.
Kabla ya kuona yaliyopatika katika yale majeneza basi tuangalie kidogo injili ya Yesu katika biblia yasemaje.
Mathayo 27:45-56 inaeleza hadithi ya kukamatwa kwa Yesu hadi kusulubiwa kwake. Mathayo 27:57-61 inaeleza maziko ya Yesu na Yosefu wa Arimathea hadi ilipobainika kufufuka kwake. Marko 16:19-20 inaeleza kupaa kwake Yesu kule Bethania.
Katika zile jeneza au Ossuary za udongo zilipoanza kuchunguzwa na kuoshwa kitaalamu Mambo ya ajabu yaligunduliwa.
Juu ya majeneza yaliandikwa majina ya watu waliozikwa ndani yake kwa lugha ya Kiebrania na Kigiriki. Mojawapo iliandikwa Yesu mwana wa yusufu- Jesus son of Joseph, je aliyelala humo atakuwa nani?
Huu ni ugunduzi wa kaburi yenye jeneza na ndani yake mifupa ya mtu aliyeitwa Yesu. Huu ukawa ukweli usiomezeka. Mengine ya majeneza hayo yaliandikwa kwa Kiebrania, Maria au Mariamne kumaanisha Maria Magdalene na nyingine Yusufu-. Iliaminika kuwa ilikuwa makaburi ya familia Yesu.

Ugunduzi huu haukupewa mashiko sana na kwa hivyo utafiti wangu nitafikia hapo ili nisiwe chanzo cha kuteteresha imani ya mtu.
Lakini itakuwaje Yesu kukamatwa,kusulubiwa,kutokezea wanafunzi wake na kupaa kwa baba yake juu mbinguni na mabaki yake kupatikana?

Leave a comment