IPI SURA YA YESU?

Karibu kila mtu ana dhana fulani kuhusu muonekano wa Yesu Kristo. Unapoenda nyumba yoyote,taasisi,kanisa na kwingine utapata picha ya yesu ukutani.

Yesu ndiye mtu aliyechorwa zaidi katika sanaa ya Magharibi. Picha zake hutambuliwa kwa urahisi, ambapo huoneshwa akiwa na nywele ndefu na ndevu, akiwa amevalia vazi ndefu lenye mikono mirefu linalofanana na kanzu (sana la la rangi nyeupe), na pia akiwa amejifunga joho (sana la rangi ya samawati). Muonekano wa Yesu umefahamika sana na wengi kiasi kwamba unaweza kutambuliwa ukiwa hata kwenye mikate au biskuti. Lakini je sura ya Yesu ni ipi?

Mwaka wa 1979 Filamu iitwayo Yesu ilitolewa ikiongozwa na Peter Sykes na John Krish. Mhusika mkuu ni muigizaji wa uingereza Brian Deacon. Filamu hiyo inaangazia maisha ya Yesu hadi kupaa kwake mbinguni kwa kuzingatia injili ya Luka.Usimulizi wa sauti wa mara kwa mara unaangaziwa ikieleza usuli wa Yesu. Basi tangu kuwepo kwa Filamu hiyo watu wamechapisha picha ikionyesha Brian Deacon kama yesu.

Filamu,iitwayo YESU-Mhusika mkuu Brian Deacon.
Brian Deacon.
Brian Deacon..
Brian Deacon.

Mwaka wa 1977 Filamu nyingine ilitolewa iitwayo Yesu wa Nazareti.Mhusika mkuu aliitwa Robert Powell na kuongozwa na Franco Zeffirelli. Filamu hii pia inaangazia maisha nzima ya Yesu. Baada ya kuolewa Filamu hi pia watu walichukulia Robert Powell kama Yesu na kuchapisha picha zake.

Filamu,iitwayo YESU WA NAZARETI- Mhusika mkuu Robert Powell.
Robert Powell.
Robert Powell.
Robert Powell.
Robert Powell asema yeye si Yesu Bali ni muigizaji wa filamu.

YESU NI NANI?
Yesu alizaliwa takriban miaka 2000 iliyopita na alikuwa myahudi. Katika picha tunayoona sasa ni kwamba inaonyesha wale waigizaji wa Filamu kama Brian Deacon na Robert Powell na wengineo. Yesu anachorwa akiwa amevaa kanzu ndef

Lakini je, alikuwa anafanana hivi kweli ? Huenda sivyo.
Kwa kweli sura hii inayotambuliwa huenda ilibuniwa karne nne baada ya kuzaliwa kwake , nyakati za Ufalme ya Byzantium.Usanii wa wakati huo ulikuwa usanii elezi tu, sio ya uhalisi.
Usanii huo ulifanya kwa taswira ya ufalme wa kirumi, tunavayoona kwa mchoro wa kanisa la Santa Pudenziana iliyoko jijini Rome Utaliana.
Lakini sura yake haswa ilikuwaje?

Picha ya Yesu,Rome.

1.Nywele na Ndevu.
Wakato wakristo wa zamani hakuwa wanamuonyesha kama Mungu, walieleza kuwa Yesu alikuwa tu binadamu kama mwengine, bila ndevu na mwenye nywele fupi.Katika karne ya kwanza wakati wa Ufalme wa Ugiriki na warumi, wanaume walitakiwa kuwa na nywele fupi.Hata wanafilosofia walinyoa nywele zao.Kwa hivyo Yesu, kama mwana filosofia, huenda pia alikuwa na ndevu fupi, na pia huenda nywele yake haikuwa ndefu kama vile tunavyodhania.

2.Mavazi.
Wasanii wa Byzantino walimchora Yesu kama mdogo wake Zeus, mungu wa Kigiriki. Wasanii wa Byzantino walimchora Yesu kama mdogo wake Zeus, mungu wa Kigiriki.Wakati wa Yesu, mabwanyeye walivalia kanzu wakati wa sherehe maalum ili kuonyesha ukubwa wao .Katika Biblia, Yesu pia aonya kwenye mafunzo yake, alipokuwa akifundisha, Yesu alisema,
“Jihadharini na walimu wa sheria”.”Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu na kusalimiwa kwa heshima masokoni.”Miguuni Yesu huenda alivaa lapulapu.Pia wao hupenda kukaa viti vya mbele katika masinagogi na kupewa nafasi za he shima katika karamu.”
(Marko 12; 38-39).
Matamshi ya Yesu huaminika kuwa ya kweli kwenye vitabu vya Injili, kwa hivyo twaezang’amua kuwa Yesu mwenyewe hakuvalia kanzu.

3. Miguu.
Miguuni Yesu huenda alivaa lapulapu.Kila mtu alikuwa akivaa lapulapu wakati huo.

4.Sura.
Yesu alikuwa Yahudi.Kwa hivyo alifananaje kama myahudi mwenye miaka thelathini alipoanza kuhubiri kama ilivyonenwa katika kitabu cha Luka?
Maelezo ya picha,Kwa hivyo alifananaje kama myahudi mwenye miaka thelathini alipoanza kuhubiri kama ilivyonenwa katika kitabu cha Luka?
Kwa hivyo alifananaje kama myahudi mwenye miaka thelathini alipoanza kuhubiri kama ilivyonenwa katika kitabu cha Luka?
Mnamo mwaka wa 2001 mwanasayansi Richard Neave aliundia BBC umbo la mwana Galilaya, kwa kipindi kilichoitwa “Mwana wa Mungu.’Hakusema ilikuwa sura yake Yesu.Ila umbo hilo lilikuwa la kuwapa watu taswira ya mwanaume kama Yesu nyakati na karne aliyokuwa hai.

Baadaye kundi la Wanasayansi kama vile Richard Nieve na Joan Taylor walijaribu kuchora picha Ya Yesu. Inasemekana kuwa Richard

Swala la ipi sura ya Yesu sitoweza kujibu ila najua jibu. Kwa hivyo usingoje kuona Yesu kama ulivyozoea atakaporudi! Mpaka sasa swala la ipi sura ya Yesu imebaki Kitendawili!

Akubariki Rabana kwa imani yako🙏



Leave a comment

About Me

Welcome to my blog, MTU KUZI, a space dedicated to informing and educating a diverse audience without bias toward age, gender, race, or any other distinguishing factor. I am a seasoned professional with a deep foundation in communication, translation, administration, and education. My extensive experience spans prestigious roles at institutions like Pwani University, Mozilla Foundation, KIPPRA, and teaching Kiswahili at the University of Carolina – Chapel Hill.As a Kiswahili expert, I specialize in translating between English and Kiswahili and tutor both languages with a focus on immersive, practical learning experiences. My expertise in Kiswahili not only enhances my teaching but also enriches my translations, allowing for culturally and contextually accurate communication.In this blog, I leverage my skills and experiences to create content that bridges cultural divides and fosters understanding. Proficient in various software applications and online collaboration platforms, I aim to streamline communication processes and engage with a global audience effectively.You are invited to join me on this journey of exploration and learning. Follow MTU KUZI on Facebook, Twitter, Instagram, and LinkedIn to stay updated and connected. Thank you for visiting, and I look forward to sharing more with you.

Newsletter