Siku ya wajinga duniani -inayoadhimishwa Aprili 1 kila mwaka – imekuwa ikiadhimishwa kwa karne kadhaa na tamaduni tofauti, ingawa asili yake halisi bado ni siri.
Mila ya Siku ya wajinga ni pamoja na kuwadanganya watu au kuwafanyia au utani wa vitendo mbalimbali.
Wakati historia yake halisi imeghubikwa na siri, kukumbatiwa kwa utani wa Siku ya Wajinga ya Aprili Mosi na vyombo vya habari kumehakikisha maisha marefu ya likizo hii isiyo rasmi.
Je siku hii iliasisiwa lini na kwa madhumuni gani?
Siku hii ilianzaje?
Baadhi ya wanahistoria wanakadiria kwamba ya Siku ya Wajinga ilianza mwaka 1582 wakati ambapo Ufaransa ilibadili kalenda ya Julian na kuhamia kwenye kalenda ya Gregorian.
Kubadilika huku kwa kalenda kulibadilisha tarehe za mwaka na hivyo nchi hiyo ikaanza kusherehekea mwaka mpya Januari Mosi badala ya Aprili.
Lakini kwa bahati mbaya maamuzi hayo ya kubadili kalenda ya mwaka yaliyofanywa na Papa Gregory wa 13, hayakuwafikia wananchi wote wa Ufaransa na badala yake baadhi wakaendelea kusherehekea mwaka mpya Aprili Mosi. Hivyo basi waliosherehekea mwaka mpya Aprili Mosi, waliitwa wajinga na siku hiyo ikaitwa ya wajinga.

Watu ambao walichelewa kupata habari au walishindwa kutambua kuwa mwanzo wa mwaka mpya ulikuwa umehamia Januari 1 na waliendelea kuusherehekea katika wiki ya mwisho ya Machi hadi Aprili 1 wakawa wanafanyiwa utani na wongo wakiitwa “Wajinga wa Aprili.
“Mizaha hiyo ilikuwa ni pamoja na kuwekewa karatasi zilizochongwa kwa muundo wa samaki migongoni mwao na akiitwa “poisson d’avril” (samaki wa Aprili), iliyosemekana kuashiria samaki wachanga, waliovuliwa kwa urahisi na mtu anayeweza kuhadaiwa kwa urahisi.
Wengine wanaihusisha siku hii na sherehe za Warumi zilizoadhimishwa Aprili Mosi ambapo watu walivaa nguo za ajabu na za kuchekesha wakati huo, ilianza kusherehekewa Machi 25 na kumalizika Aprili Mosi.
Baadhi ya wanahistoria wa Uingereza wameihusisha sikukuu hii na sherehe zinazofanywa kila Aprili Mosi nchini India ambapo watu walirushiana vitu na kuchafuana kwa keki au rangi kama sehemu ya utani.
Siku ya wajinga duniani ilienea kote Uingereza wakati wa karne ya 18. Huko Scotland, mila hiyo ikawa hafla ya siku mbili, ikianza na watu kutumwa kufanya vitu mambo yasiyowezekana na hata wengine kuwekewa mabango kama ya ‘nipige’ mgongoni’ au kuwekewa mikia bandia.

Mashirika makubwa yaiendeleza
Kama ilivyo siku ya afya duniani baadhi ya taasisi kubwa duniani nazo huadhimisha Siku ya Wajinga na kuwaweka mtegoni maelfu ya watu.
Mwaka 1957 Televisheni ya Uingereza (BBC), ilionesha kipande kifupi cha video katika kipindi cha Panorama kinachoonesha wakulima huko Uswisi wakivuna tambi (spaghetti). Dakika chache baada ya video hiyo kurushwa, mamia ya wananchi walijaa katika ofisi za shirika hilo la utangazaji wakitaka kujua aina hiyo ya kilimo cha tambi.
Mwaka 2008, BBC kwa mara nyingine walirusha video fupi iliyoonesha pengwini(ndege mnene wa (majini asiyeweza kuruka juu)wakiruka angani na taarifa hiyo ilieleza kuwa wanyama hao wanakimbia hali ya hewa ya bara la Antaktika na kwenda Amerika ya Kusini. Kiasili, pengwini hawezi kuruka.

Mnamo mwaka wa 1992, Redio ya Kitaifa ilitangaza kwamba Rais wa zamani Richard Nixon alikuwa akiwania urais tena… hata hivyo ukweli ni kwamba aliyekuwa akizungumza alikuwa ni mwigizaji tu na , sio Nixon, na sehemu hiyo ilikuwa kisa cha wongo kuwapumbaza watu siku hiyo ya wajinga duniani .
Mwaka wa 1996, kampuni inayomiliki migahawa ya Taco Bell, iliwahadaa watu kwamba imekubali kununua Kengele ya kihistoria ya Liberty Bell huko Phidalphia na ingebadilisha jina la kengele hiyo ili kuitwa Taco Liberty Bell.
Kwa mtu wa kawaida ,jihadaria usije ukatiliwa chumvi kwenye chai na sukari mchuzini.Kunao pia wanaovusha mipaka na kuongeza pilipili katika poda ya kujipodoa ili kuwanasa kuwana ‘watakaopatikana kuwa wajinga wa Aprili.
NIFUATE KWENYE MITANDAO # NICHOLAS ROP #PROFESA KIJANA MPEKUZI.
AKUBARIKI MWENYEZI MUNGU🥰

Leave a comment