Leo alfajiri nimerauka kama kawaida lakini nimeshangazwa kwamba gonjwa la SARATANI imeweza kupata wanawake wengi Kaunti ya Kilifi na maeneo mengi duniani. Nimeamua kuchunguza kuhusu janga hili na nimepata haya.
SHINGO YA KIZAZI
SHINGO YA KIZAZI NI NINI?
Shingo ya kizazi (cervix) ni kiungo cha mwili kinachopatikana kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke. Ni sehemu ya mji wa mimba (Uterus) inayotokezea kwenye uke (tupu) wa mwanamke. Tazama picha ifuatayo

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI?
Ni mabadiliko hasi (yasiyo ya kawaida) ya chembechembe hai zilizopo kwenye shingo ya kizazi. Mara nyingi saratani hii ikiwa inaanza haionyeshi dalili yoyote hivyo mgonjwa hawezi kuchukua hatua yoyote kukabiliana na tatizo hili kwa wakati huu.
Kwa kiasi kikubwa saratani hii husababishwa na maambukizi ya mda mrefu (persistence infection) ya virusi viitwavyo Human papilloma, ambavyo huenezwa kwa njia ya kujamiiana. Kawaida mwili una uwezo wa hudhibiti maambukizi haya yaingiapo mwilini, lakini yasipodhibitiwa kikamilifu na kuwepo mwilini kwa mda mrefu husababisha ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.
MAMBO MENGINE YANAYOCHANGIA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
- Kufanya ngono zembe
- Kuwa na wapenzi wengi
- Kukoma siku katika umri mkubwa
- Utumiaji mafuta mengi katika chakula.
- Kutokufanya mazoezi ya mara kwa mara.
- Unene kupita kiasi
- Uvutaji sigara.
- Utumiaji wa pombe kupita kiasi.
- Historia ya saratani ya matiti katika familia.
DALILI ZA UGONJWA WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
Dalili za ugonjwa huu huanza kujitokeza baada ya tatizo kuanza kukomaa, zifuatazo ni baadhi ya dalili
- Kutokwa na maji maji yenye harufu ukeni
- Kutokwa damu baada ya kujamiiana
- Kutokwa damu kusiko kwa kawaida (siyo damu ya hedhi)
- Kuumwa mgongo na kiuno
- Kuumwa miguu
- Kizunguzungu na kuishiwa nguvu
NINI KIFANYIKE?
Saratani ya shingo ya kizazi inazuilika au kutibika kabisa endapo itagundulika ikiwa kwenye hatua za awali.
Hivyo ni muhimu kufanya uchunguzi wa afya yako kwa kadiri utakavyoshauriwa na wataalam wa afya
Wanawake wote walio na umri kuanzia miaka 30 na kuendelea wanatakiwa kufanya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi.
Kumbuka: Wakati wa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi ni sasa usisubiri hadi uone dalili, fika kituo cha huduma za afya kwa ushauri/mwongozo Zaidi.
UCHUNGUZI WA SARATANI YA MATITI KWA AKINA MAMA
(BREAST CANCER)
SARATANI YA MATITI NI NINI?
Ni mabadiliko ya chembechembe hai zilizopo kwenye matiti saratani hii kwa kawaida haina dalili katika hatua za mwanzo. Wanawake katikahatua za mwanzo za ugonjwa hawana maumivu au dalili nyingine zozote.
Uchunguzi wa awali ndio utakao wezesha kuugundua ugonjwa katika hatua hii mabadiliko yaletwayo na saratani ya matiti.
- Kivimbe katika titi au kwenye makwapa.
- Mabadiliko ya umbo na ukubwa wa titi.
- Kutokwa na majimaji au damu katika chuchu ama chuchu kuingia ndani ya ziwa.
- Mabadiliko katika rangi ya ngozi ya titi (kuonekana kama sehemu ya nje ya ganda la chungwa).
MAMBO YANAYOCHANGIA KUPATA SARATANI YA MATITI
- Jinsi ya kike
- Kuanza hedhi katika umri mdogo.
- Kukoma siku katika umri mkubwa
- Kutozaa kabisa.
- Kutonyonyesha kabisa au kunyonyesha kwa muda mfupi.
- Utumiaji mafuta mengi katika chakula.
- Kutokufanya mazoezi ya mara kwa mara.
- Unene kupita kiasi
- Uvutaji sigara.
- Utumiaji wa pombe kupita kiasi.
- Historia ya saratani ya matiti katika familia.
JINSI YAKUJILINDA NA SARATANI YA MATITI
- Kujichunguza mwenyewe mara kwa mara kwa mara.
- Uchunguzi wa kitabibu wa matiti kila mwaka.
- Uchunguzi wa matiti kwa njia ya mashine ya mionzi (mara moja kwa mwaka kwa wenye miaka zaidi ya 40).
- Wanawake wote wenye umri kuanzia miaka 21 wajichunguze matiti yao siku ya 5-7 baada ya kumaliza hedhi mbele ya kioo.
HATUA 5 RAHISI ZA KUJICHUNGUZA MATITI
- Jiangalie katika kioo ukiwa umesimama wima na umeweka mikono kiunoni.
- Angalia kama kuna mabadiliko katika umbo au rangi ya ngozi ya titi na kama
AU
- Ukiwa umesimama au umelala chali tumia mkono pamoja na kipaji cha vidole vya mkono wa kulia kuchunguza titi la kushoto na mkono wa kushoto kuchunguza titi la kulia kwa njia ya mzunguko.
- Kwa upole kamua chuchu ya kila titi na chunguza kama kuna ute ulio changanyika na damu.
- Muone daktari kama kuna uvimbe au ute ulio changanyika na damu au hali yoyote ulioiona wakati wa kujichunguza.

Leave a comment